OMAN STUDIES CENTRE
for Documentation and Research on Oman and the Arabian Gulf
(Kituo cha Elimu cha Omani -
kwa Nyaraka na Utafiti kuhusu Omani na Ghuba)
[Deutsch] -
[English] -
[Español] -
[Français]
NIA NA MADHUMUNI
Kituo cha Elimu cha Omani (Oman Studies Centre) kilianzishwa nchini Ujerumani mwaka 1975 kama
kituo cha nyaraka kuhusu Omani na Ghuba.
Ni kituo kinachojitegemea, kisichokuwa cha kiserikali na ni taasisi ya Elimu
isiyokuwa ya kibiashara, ambayo kazi yake kubwa ni kukusanya habari kuhusu
Omani, kusaidia na kuhakiki utafiti kuhusu Omani na kuukuza ili watu
waipende Omani, Sambamba na mtazamo wa fani mbalimbali za kituo hiki. Nyanja
zinazopendelewa ni pamoja na Historia ya Omani kwa upana zaidi, Jiografia,
Utamaduni, Uchumi, Sanaa, Sheria, Lugha, Historia ya asili na hata inajumuisha
mada ndogondogo, kama vile ukusanyaji wa Stempu na medali za zamani.
Kituo cha Elimu cha Omani kinalenga Hasa katika:
- Kuhimiza masomo kuhusu Historia ya Omani na ya jamii yake, Uchumi na hali ya kijamii katika Usultani wa Omani
- Kuwezesha watu kupata habari za Omani na kuzichapisha
- Kukusanya nyaraka za rejea na kutayarisha nyaraka kuhusu Omani
- Kukuza na kuhakiki utafiti kuhusu Omani
- Kutoa habari sahihi na za karibuni kabisa kuhusu Omani kwa watafiti, Wasafiri, Waandishi wa Habari na wafanyabiashara.
ENEO
Maeneo ya Kijiografia yaliyolengwa na Kituo cha Elimu cha Omani ni yale ya
Usultani wa leo wa Omani, sambamba na maeneo ambayo kihistoria yalikuwa
chini ya Omani. (Kama vile Suahil Uman - Inayojulikana kwa sasa kama UAE,
Mwambao wa Makran wa Irani na Pakistani, Zanzibar (Unguja, Pemba) na Mwambao wa Afrika
Mashariki (Mombasa, Kilwa, Lamu, Pate, ...).
VIFAA / ZANA
Kituo kinayo maktaba mahususi yenye makusanyo maalum kama vile nyaraka za
vipande vya magazeti, Kadi za orodha ya majina ya vitabu (katalogi),
kumbukumbu za vitabu na habari nyingine.
Toleo hili la ukurasa wa WEB ni hatua ya kwanza kuelekea mabadiliko kwa
Kituo cha Elimu cha Omani kuwa kituo halisi cha Nyaraka (angalia vilevile
Oman Internet Project page [ukurasa wa mradi wa mtandao wa mawasiliano kutumia kompyuta - Internet - wa Oman] ).
HUDUMA
Sehemu hii bado inatayarishwa, kwa mantiki hiyo nyaraka na habari zetu
muhimu na nyingine bado haziwezi kupatikana kupitia Internet. Kwa wakati
huu tunakuunganisha na vitu vingine kwenye Internet kuhusu Oman na
tunakualika kujiunga na Juhudi zetu za kukijenga kituo kamili cha Nyaraka
juu ya Omani.
Kwa maelezo zaidi kuhusu Omani kwenye Mtandao wa Kompyuta (Internet)
Unataka kuona kwa haraka ni nini kimebadilika kwenye ukurasa wetu wa Mtandao
wa mawasiliano kutumia Kompyuta (WEB) tangu ulipoutembelea kwa mara ya mwisho?
Basi nenda kwenye Oman Update Newsletter #11 (taarifa za hivi karibuni kabisa za Omani) au angalia kwenye habari za nyuma.
Je kuna muunganisho unakosekana? Je Kuna muunganisho ambao umepitwa na wakati?
Tunakaribisha maoni na ushauri wako kuhusu kurasa ambazo ungependa kuziona
zimeorodheshwa kwenye ukurasa wetu wa WEB.
Tafadhali tuma ujumbe wako wa E-mail kwa omandoc@pobox.com.
Hakuna mawasiliano ya E-mail? Basi acha maoni yako kwenye Kitabu cha wageni.
Imetengenezwa : Septemba 1996; na kukarabatiwa tena Julai 10, 1999. -
Haki zote zimehifadhiwa Copyright © 1996-1999 by Oman Studies Centre.
We promote ISO-8859-6 Arabic standards